Jumatano, 14 Agosti 2013
VIKOSI VYA USALAMA NCHINI MISRI
Vikosi vya usalama nchini Misri vimevamia kambi mbili za wafuasi wa Raisi aliyepinduliwa Mohammed Morsi mjini Cairo,kukiwa na taarifa za watu wengi kuuawa.Watu walioshuhudia wanasema wameona takribani maiti 40,lakini kundi la Ndugu wa Kiislamu Muslimu Brotherhood linasema mamia ya watu wamekufa.Tingatinga za kijeshi zilivamia kambi kuu nje ya msikiti wa mashariki wa Rabaa al-Adamiya pamoja na kambi ya medani Nahda nayo ilivamiwa huku waandamanaji wakipewa matibabu pembeni ya maiti katika hospitali za dhalula pia bint wa miaka 17 wa mfuasi mashuhuli wa Muslimu Brotherhood,Mohammed el-Beltagy alipigwa Risasi.Na mpiga picha wa sky news Mick Deane, nae pia ameuawa katika ghasia hizo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni