Jumatano, 14 Agosti 2013

JESHI NIGERIA "lamua" KAMANDA WA BOKO HARAM

Jeshi nchini Nigeria limetangaza kuwa limemuua kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la Boko Haram.Taarifa hizo za kijeshi zimesema kuwa kiongozi huyo aliyeuwawa ni Momodu Bama ambaye ni wapili katika uwongozi wa kundi hilo la wapiganaji. Mapema mwizi huu wafuasi wengine wakundi hilo la Boko Haram ambao walikuwa wanakamatwa walifichua kwamba huyo kamanda wao alikuwa ameuwawa.Msemaji wa jeshi Brig Jenerali Chris Olukolade amesema Momodu Bama ambaye pia anafahamika kama "Abu Saad",alikuwa naujuzi wa kufyatua makombora ya kutungulia ndege. Mapema mwezi wa mei,Nigeria ilitangaza hali ya hatari kaskazin mashariki mwa nchi ilikupambana na wapiganaji hao wa Boko Haram.Hata hivyo hadi sasa hakuna taarifa huru kuthibitisha kuuwawa kwa Bwana Momodu Bama nao Boko Haram wenyewe hawaja thibitisha kifo cha kiongozi huyo.Jenerali Olukolade,alisema Momodu Bama alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Boko Haram waliokuwa wakitafutwa zaidi na kulikuwa kuna zawadi ya dola $155,000,£100,000 kwa yeyeto atakayetoa habari

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni