Ijumaa, 30 Agosti 2013
KANALI FEKI WA JESHI ANASWAA...
Ibrahim Moses mkazi mwenge jijini Dar es salaam amenaswa na polisi wakituo cha mwenge kwa madai ya kujifanya askari wa jeshi la wananchi (JWTZ) mwenye cheo cha kanali. Kijana huyo alinaswa na polisi kwa kushirikiana na maafisa wa JWTZ baada ya kuwekewa mtego kutokana na kudaiwa kuwa alikuwa anajiita kanali Ibra,hivyo kutiliwa mashaka hasa baada ya siku moja kuonekana napingu. Habari za kipolisi zinadai kuwa Ibra alikuwa akifika kituo cha polisi mwenge mara kwa mara na alikuwa akipewa heshima zote kama afisa wa jeshi na hasa kwa kuwa alikuwa akitoa ushirikiano wakati wa kunasa wahalifu. "Alikuwa akija kituoni na kujifanya ni kanali Ibrahimu akiwa na gari lake,hivyo huripaki na kupatiwa ulinzi mpaka shughuli zake zitakapo kwisha maeneo hayo."Ilikuwa akikuta watu wamejazana hapo kituoni alikuwa mkali na kuhimiza washuhulikiwe haraka kwani hapendi kuona watu wamejaa kwenye kituo;Kilisema chanzo chetu kituoni hapo.Walimtilia mashaka baada ya kukutwa napingu yeye akiwa kama kanali tena wa JWTZ.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni